Jeremiah 8:4-6

Dhambi Na Adhabu

4 a“Waambie, ‘Hivi ndivyo asemavyo Bwana:

“ ‘Je, watu wanapoanguka hawainuki?
Je, mtu anapopotea harudi?
5 bKwa nini basi watu hawa walipotea?
Kwa nini Yerusalemu inapotea kila mara?
Wanangʼangʼania udanganyifu
na wanakataa kurudi.
6 cNimewasikiliza kwa makini,
lakini hawataki kusema lililo sawa.
Hakuna anayetubia makosa yake
akisema, “Nimefanya nini?”
Kila mmoja hufuata njia yake mwenyewe
kama farasi anayekwenda vitani.
Copyright information for SwhNEN